EPHRAIM SEKELETI-EASTER CONCERT 2012 - BY MSAMA PROMOTION

Monday, July 23, 2012

JAMES TEMU (UNCLE JIMMY), BAHATI BUKUKU, RULEA SANGA (BLOGER), DAVID ROBERT NA WENGINE KUJA NA FILAMU KALI YA KUMTUKUZA MUNGU WETU "DUNIA HAINA HURUMA"

Mwandishi: Rulea Sanga

Mshiriki mwingine wa filamu ya "Dunia haina Huruma", Blogger wa RUMA AFRIKA, Rulea Sanga. Hapa akiwa katika gari la Wise Men wa Nabii TB Joshua katika Synagogue ya THE SCOAN. Kumbuka mwezi Aprili 2012 aliitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazi yake nzuri ya blogu yake ya www.rumaafrica.blogspot.com

Umefika wakati Mungu amezungumza na hawa watumishi wa Mungu kwa kuwapa maono ya kutengeneza filamu ya "Dunia Haina Huruma". Ujumbe huu unatoka katika nyimbo mpya ya mwimbaji maarufu Tanzania, Bahati Bukuku inayoitwa "Dunia haina Huruma" Nyimbo hii imekuwa gumzo jijini Dar es Salaam kutokana na ujumbe wake unaogusa maisha ya watu na kukuweka karibu sana na Mungu unapousikia. Kama hujawahi kuusikia, nakuomba ujitahidi kusikiliza Praise Power Radio na Wapo Radio utabarikiwa.

Mhusikaka mkuu wa filamu hii, Bahati Bukuku

Kutoka na wimbo huu, watumishi wa Mungu wameamua kukaa chini na kuuzambaza ujumbe huu kwa njia ya filamu. Kwahiyo utafaidika kuusikia kwa njia ya uimbaji na pia kwa njia ya maigizo.

Katika filamu hii kutakuwa na watumishi wa Mungu kama James Temu a.k.a Uncle Jimmy (ambaye ni mwigizaji wa filamu Tanzania na ni mtangazaji wa Praise Power Radio Tanzania, mbali na hapo ni blogger) , Rulea Sanga (ambaye ni blogger na ni graphic designer, na mwezi April 2012 alibahatika kuitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazii yake nzuri ya blogu), David Robert (huyu ni muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na ni mjasiliamali mkubwa sana Tanzania), Bahati Bukuku (Huyu ndiye mhusika mkuu wa filamu hii, ni mwimbaji wa nyombo za injili Tanzania na amekuwa baraka kwa wale waliosikia nyimbo zake), Riyama Ally (huyu ni mwigizaji wa filamu Tanzania, amefanya kazi nyingi katika uigizaji)

Wimbo wa Bahati Bukuku wa Dunia haina huruma unagusa sana mioyo ya watu, hasa wale walioko katika ndoa na wale wanaotaka kuingia katika ufalme wa ndoa. Kutokana na wimbo huo, mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku akaamua kuja na wazo la kutengeneza filamu ambayo itaonyesha kila kitu alichokiimba katika wimbo huo.

Mshiriki mwingine wa filamu ya "Dunia haina Huruma", Blogger wa RUMA AFRIKA, Rulea Sanga. Hapa akiwa katika gari la Wise Men wa Nabii TB Joshua katika Synagogue ya THE SCOAN. Kumbuka mwezi Aprili 2012 aliitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazi yake nzuri ya blogu yake ya www.rumaafrica.blogspot.com

Kwa sasa kila kitu kuhusina na filamu hii kimeandaliwa, ila kilichobaki ni kumtafuta dada mrembo na mwenye kuvutia, kwani kuna sehemu inahitajika kwaajili ya dada ambaye ni mrembo sana. Kama wewe unajiona ni mrembo na uunajiamini na unaweza kuigiza tunaomba uwasiliane kwa namba hii +255 713-763939.


Kumbukeni haya yote yanafanyika kwaajili ya kumtangaza Kristo na kuonyesha kuwa hata sisi tuliokoka tunaweza kufanya vitu vikali na vizuri. Umefika wakati wa kupenda vilivyo vya Mungu na ku-support kazi ya Mungu. Support yako itatuwezesha kufanya vitu vikali. Mungu anatumia watu kufanikisha kile anachotaka kifanyike, na leo wewe utakuwa ni mmoja wa wale Mungu anapenda ushiriki katika ku-support kazi hii isonge mbele. Kama unamchango wako wowote tutashukuru sana kusikia na kupokea kwako, mchango unaweza ukawa na mawazo, fedha au vitu. Kama wewe ni mmiliki wa vyombo vya shooting unaweza ukajitokeza tukafanya kazi ya Mungu.

Kwa mujibu wa Bahati Bukuku, amesema filamu hii itakuwa ya utofauti na filamu za watu wengine kwani watu watakao shiriki filamu hii watapimwa uwezo wao wakufanya kazi napia watasafiri baadhi ya mikoa kukamilisha kusudio la filamu hii.
Wadau wa blogu hii endeleni kuitembelea, ili mfahamu kitu kinachoendelea.

Riyama Ally ni mtumishi wa Mungu na anacheza filamu za Kitanzania (Bongo Movie). Naye atashiriki katika filamu hii.

David Robert, ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na mjasiliamali. Atashiriki
Uncle Jimmy , ni mwigizaji katika Bongo Movie na amecheza na waigizaji wakubwa Tanzania akiwaomo Ray, JB,O na wengine wengi. Katika filamu hii utaona kazi yake ya uigizaji katika muonekano mwingine.


NIKUPE KIONJO CHA TAMTHILIA

Bahati Bukuku alipigiwa simu na mwanamke mmoja ambaye alijitambuliha kuwa yeye ni mke mwenzake, alimpa taarifa mbaya akimwambia "Nenda kachukue mzoga wako Muhimbili" . Bahati Bukuku akiwa katika kutafuta marafiki zake kuulizia taarifa hizi ili kujua zaidi, aliamua kufika mochwari Muhimbili, na alipofika Muhimbili alikutana na taarifa mbaya za kuumiza moyo wake kutoka kwa wale waliokuwa hapo Muhimbili.
Bahati Bukuku aliingia chumba cha maututi na kuona mpenzi wake amepoteza fahamu na hawezi kumtazama. Nilijisemesha kuwa "Dunia haina huruma, haina fadhili, nani mwenye huruma anifariji, moyo unavuja damu kwa matatizo ninayopata."
Bahati Bukuku akamua kuwapigia ndugu wa mume wake Mbeya ili awaeleze yaliyomsibu, lakini cha kushangaza ni kwamba wote walimsusia. Akajaribu kuchukua kitabu cha Bank ili kuangalia kama kuna pesa kidogo zimsaidie, lakina cha kusikitisha anaona ATM haizomi nikimaanisha hakuna pesa. Hakuchoka akaenda kwa daktari na kutaka kumuuzia gari aina ya Vogi, lakini daktari anakataa na kusema haya magari yanakula mafuta sana kwahiyo sitoweza kuwa nalo. Akiangalia marafiki zake wanazidi kularua moyo wake kwa maneno makali.
Bahati Bukuku kila akimwaangalia mume wake anazidi kuchanganyikiwa na hawezi kuongea naye. Mashemeji zake hawataki kusaidia na kila akiomba msaada kutoka kwao, nao wanamwambia "Shemeji sisi tunaenda kuangalia mpira Ulaya" akiwaambia mawifi zake nao wanamwambia, "Wifi hatuwezi kukusaidia, tunaenda kucheza segere".
Bahati Bukuku akaamua kwenda tena kwa daktari kuomba asaidiwe. Na chanzo cha matatizo kikaanza hapo. Bahati akibdi azae na huyu daktari ili apate msaada, maana amehangaika sana bila ya kupata msaada, na mgonjwa hali yake ni mbaya sana.

Mzigo ukazidi kwa Bahati Bukuku, hali ikazidi kuwa mbaya sana, maana amefanya kosa la kufanya tendo la ndoa na daktari na kuzaa mtoto, na bado ndugu hawampendi.
Baada ya kupata nafuu kwa mgonjwa na kurusiwa nyumbani na kuendelea na maisha yake ya kwaida, Bahati Bukuku akamwambia kuwa nimezaa na daktari. Na hii nililifanya kutokana na kushindwa kupata msaada kutoka kwa ndugu na marafiki, wote walinikimbia, kwahiyo nikaamua kufanya hivyo kwa daktari ili nipate pesa ya kukusaidia upate matibabu.

Mume na Bahati Bukuku aliposikia habari hizo kuwa mke wake ana mtoto na daktari akachukua mapnga na kutaka kumuua.

Mume na Bahati aliondoka na baadae Bahati Bukuku akaitwa kijijini kwa mume wake. Alipofika kijijini akawasalimia, nao hawakuta kumjibu wala kumsikia. Kikao kikakaa kutaka kumhukumu, na wakamwambia Bahati Bukuku, "Kama unataka kuishi katika familia hii, mtoto auawe". Akamtazama mume wake na yeye akamtazama kwa hasira. Bahati aakjiuliza, amkimbile nani kwani ndugu, marafiki na mume wake hawamtaki.
Ndugu wakmuweka mtoto kati ili wampige mapanga, akatokea baba mmoja na kuwauliza, ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kupiga panga huyu mtoto. Mume na Bahati Bukuku baada ya kusikia hilo aliomba msamaha kwa mke wake na kusema kuanzia leo hii ya dunia yameisha nataka kutengeneza na Mungu.

Bahati amegundua ya kuwa Mungu anaweza kujibu maombi na kusamehe. Hii ni stori fupi ya tamdhilia ambayo itakujia kwako, kuna mengi ambayo utayaona katika filamu hiyo, Utaona mazingira yatakyotumika, wahusika wanatavyokuwa serious kukuletea huu ujumbe.

Lakini nataka kukuuliza wewe mdau wangu, unafikiri Rulea Sanga, David Robert, Uncle Jimmy, Bahati Bukuku n, Riyama Ally anaweza kufaa katika kitengo kipi?

Kwa haraka haraka kuna wahusika wafuatao:

1. Mke wa yule mume mgonjwa
2. Mume ambaye ni mgonjwa
3. Dada aliyempigia simu mke wa yule mume
4. Marafiki /mashoga wa mke wa mume
5.Daktari
6. Ndugu wa mume
7. Watu waliokataa kumsaidia Bukuku akiwa na shida.
8. Ndugu aliyepigiwa simu na Bahati Bukuku
9. Wacheza segere
9. Ndugu waliomua kwenda Ulaya kuangalia mpira
10. Mtoto wa daktari ambaye aliambiwa akatwe mapanga
11. Mtu aliyewambia wasimkate mapanga
TUNAOMBA MAONI YAKO.

FILAMU YA "SIKU YA MWISHO-666" KUWA SOKONI WIKI HII

Source: Ruma Africa & Papa Sam

(Kuhusiana na habari zingine kuhusiana na hii filamu tembelea www.rumaafrica.blogspot.com na www.samsasali.blogspot.com. Tutatakuwa tunakuletea kinachoendelea)

Ile Filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa hususani Jamii Ya Kikristo Ya Siku za Mwisho inakamilika wiki hii na Kabla ya Kuingia Sokoni Mapema Mwezi Ujao.
Katika Filamu hiyo ya kibongo ambayo Papaa Ze Blogger amecheza kama Apostle P Nizo, ambaye ni Mtume na Nabii mwenye Kanisa lenye Ishara na Miujiza mingi na Baraka kadha wa Kadha pasipo waumini wa Kanisa hilo kutambua kuwa Apostle Nizo ana "Source Of Power" isiyotoka Juu.
Filamu hiyo yenye maudhui ya Kuwakumbusha Wakristo kuhusu Siku Za Mwisho na Kurudi Kwa Yesu Kristo imesheheni Vipaji Lukuki Vya Wakristo Katika kufikisha Ujumbe kwa Jamii.

Hapa ndipo Wanapokuwa kwenye Ibada Zao Wakisali ...Its a Nice Scene

Kushoto kabisa ni Papaa Ze Blogger akicheza Kama Apostle ndani ya Scene hiyo akiwa amevaa tofauti na wengine sababu na nafasi yake katika Impact katika Jamii

Hapa Apostle Nizo Akiwa anafatilia Ibada kwa Unakini Mkubwa ndani ya Chumba Cha Siri

Hapa Papaa Ze Blogger akiecheza Kama Apostle P, akidaka "power'
Apostle P Nizo akiwa na Kisu tayari kwa Ibada Ya Sadaka....Its very interesting Scene

Wakuu Katika Katika Kujipanga Kimkakati Mara baada ya Ibada ya Chumba Cha Siri

Kulia ni Papaa Ze Blogger ambaye amecheza kama Anointed Apostle, Katikati ni Pastor Alex, ambaye amecheza kama Mfanyabiashara mkubwa ambaye pia ni Mzee wa Kanisa Wa Apostle Nizo, na Kushoto Ni Mwanadada amecheza kama Mwanaharakati wa Haki za Wanawake na Mjasiriamali ambaye yuko connected na "chumba cha siri'

Laurence akiwa mwenzake ambaye wamecheza kama Askari wanaokagua magari kama yana sticker ya 666 maana hutaweza nunua mafuta wala kuendesha gari kama haijagongwa 666.

Hawa Watu Watatu wametisha Sana katika Scene hii ya "Chumba Cha Siri" Mpaka Pastor Kaduma Mtunzi wa Filamu hiyo, na Director Wa Filamu hiyo Mr. Mtitu Wakapiga picha na Jamaa

Scene hii Jamaa akiwa ameandaa Part nyumbani kwake ambapo amealika ndugu jamaa na marafiki,

Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana wakifurahia Chakula nyumbani kwa Mtumishi ambaye baadae atabaki sababu kumbe alidai amebarikiwa na mungu kupata hela kumbe Kapiga EPA.
Shemeji Yangu Edna Luvanda akiwa ndani ya Scene ya Siku za Mwisho, Kulia ni Dorcas Sakani ndani ya Filamu.

Full Kula
Hapa Madaktari wakijiandaa ndani ya chumba Cha Operation kwa ajili ya kumuhudumia mgonjwa

Hapa Wakiendelea na Operation

Kazi Ikaendelea
 
Daktari Bingwa akiwa Kazini kwenye Scene

Wakiwa Ndani ya Chumba Cha Operation Yesu anarudi na Daktari Bingwa anatwaliwa, sokomoko waliobaki ndani ya Chumba Wamuhudumie Mgonjwa ama Wamtafute Dr. Bingwa waliyetwaliwa.