Siku ya jana 14.05.2013 Mama alishuhudia kupatika kwa baba yake aliyepotea kwa muda mrefu. Nabii Flora alimuonyesha kuwa yuko Ubungo stand. Soma ushuhuda huuu
Kushoto ni Nabii Flora, katikati ni Mzee Jackson Kisika (aliyepotea), kulia ni mwanae na Jackson kisika, dada Mary ambaye alipeleka taarifa kwa nabii Flora ukuwa baba yake amepotea
Na haya ndiyo aliyoyazungumza mwanae...
Bwana asifiwe mimi ninaitwa Mary Jackson Kisika, na huyu hapa ni baba yangu anaitwa Jackson Kisika. Baba yangu alipotea wiki moja na siku mbili. Nilikuja kwa Nabii Flora na kutaka kunitabiria kuhusiana na baba yangu alikoenda. Nabii Flora alinambia niende Ubungo nitamuona, nikamuuliza nabii . atakuwa na nani? Akanambia yupo tu anatembea tembea, anazungukazunguka. Ni liweza kwenda pale Ubungo na kuanza kumtafuta huku tukiwaonyesha watu picha. Mtu mmoja aksema hii picha tuliiona jana na baba yenu si mweusi hivi? Nikajibu ni kweli ni mweusi..akanambia ingieni kule ndani ya stendi. Tulipoenda pale h tukamuona. Tukampigia simu Nabii Flora kuwa hatujamuona, na tukarudi nyumbani. Siku ya Jumatatu niliyokuja hapa kanisani, Nabii Flora akachukua zile picha za baba yetu na kuziombea. Akasema kesho asipoonekana njooni tena nitawaelekezeni wapi mtamkuta na nitamtuma malaika wangu aende akamchukue baba yenu. Kweli siku ya Jumanne nikaja hapa, baada ya muda nikapigiwa simu kuwa baba yangu ameonekana.
Huyu baba tulimutoa katika vyombo vya habari (radio One, TBC, , tukapeleka habari katika vituo vya polisi.
Baba yetu ni baba anayetokea mkoa wa Mbeya Tukuyu. Baba yetu ana watoto ambao bado wako hai ni wanne.
Tunamshukuru Mungu wa Nabii Flora.
Wakijiandikisha kwa Nabii Flora kabla ya mahojiano na kumshukuriu Mungu.