EPHRAIM SEKELETI-EASTER CONCERT 2012 - BY MSAMA PROMOTION

Sunday, April 15, 2012


EPHRAIM SEKELETI ATOA USHUHUDA NAMNA MUNGU ALIVYOMPONYA NA UGONJWA KIPINDI ANGALI MDOGO
Ephraim Sekeleti akihudumu katika kanisa la Living water kawe-Makuti
Mwanamuziki wa Injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekeleti, jumapili ya leo tarehe 14/04/2012 alihudumu katika ibada kwenye kanisa la Living Water Kawe Makuti.Katika ibada hiyo Sekeleti aliimba nyimbo zake maarufu ikiwemo Uniongoze pamoja na nyimbo zake nyingine zilizomo kwenye album yake mpya iitwayo Acha Kulia.

Katika hali iliyoonekana kuvuta hisia za wengi kanisani hapo, ni pale mtumishi huyo ambaye ni baba wa watoto wawili alipotoa ushuhuda wa maisha yake kwa ufupi, ambapo hadi anamaliza kuusimulia watu wengi walikuwa wakilia kwa namna ambavyo Mungu alimtetea mtumishi huyo katika Maisha yake toka anazaliwa mpaka hivi leo.

Katika ushuhuda huo kwa kifupi sekeleti alisema akiwa mdogo alipata ugonjwa uliosumbua maeneo ya shingo na mdomoni, yeye pamoja na familia yake walisumbuka sana kupata matibabu, walienda sehemu zote lakini hawakupata msaada.Ilifikia hatua walienda mpaka kwa waganga wa kienyeji lakini hawakupata msaada.

Katika haali hiyo ndipo Ephraim aliweka Agano na Mungu kuwa endapo Mungu utaniponya basi nitakutumikia katika maisha yangu yote.Kwa kuwa Mungu ni mwenye nguvu alimponya Ephraim na ndipo kuanzia hapo Ephraim Sekeleti alianza kumtumikia Mungu. Mpaka sasa Sekeleti ana jumla ya album zipatazo saba ambazo ameziimba kwa Lugha za Ki-bemba,Ki-nyanja,Kiingereza na Kiswahili.

Wednesday, April 11, 2012

DAR ES SALAM -TANZANIA
I stayed in the De Monde Hotel, the building is called Benjamin Mkapa, located at the middle of  town.

THE INTERVIEW ABOUT EASTER PERFORMANCE 2012 IN DAR ES SALAAM AND DODOMA-TANZANIA
Radio Presenter was Silas Mbise from Wapo Radio FM
 From right, Wapo Radio Presenter, Silas Mbise and next International Gospel Singer, Rebeca Malope from South Africa

Tuesday, April 10, 2012

EASTER CONCERT PREPARED BY MSAMA PROMOTION - TANZANIA-2012
The concert held at National Stadium
 

Tanzania Nation Stadium 

Blogger and Marketing Manager of Glorious Celebration from Tanzania, Rulea Sanga (left )  

 
Emmanuel Mabisa (left) Music Director of Glorious Celebration from Tanzania

Gospel Singers from Tanzania - Glorious Celebration Live Band
 Just check the audience
International  Gospel Singer from South Africa, Rebecca Malope before performance

 Performing
Blogger Jimmy (right), Samsasali (left) and an entrepreneur, Hudson Kamoga